10/09/2007 |
|
|
HOME VILLAGE NEWS GRANTS ARCHIVES
;
|
MAJIMBO POLICY IN KENYA (FEDERALISM IN KENYA) Sera ya majimbo' ni siri ya maisha bora kwa kila Mkenya Monday, October 08, 2007 Daniel Ochieng’ Obunga (Kitengela, Nairobi) danobunga at yahoo dot com – 0725-408720 Sera hii ya majimbo ni swala nyeti sana wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2007 kwa vijembe vya majukwaani. Hoja kuu ya kufahamu ni kwamba chimbuko la sera ya majimbo nchini ni falsafa ya ODM ya nguvu ya umma, shirikisho pia iliunga mkono sera hii. Kwani umma ndio unapaswa kuwa na mamlaka lakini pia umma ndio unapaswa kunufaika na rasilimali za nchi. Majimbo ni moja kati ya sera za chama cha ODM nchini Kenya ambacho kitapewa kipaumbele. Jinsi vigogo vya chama walivyo ongea siku ya jumamosi Uhuru park Kuzindua kampeni ya Urais Mheshimiwa Raila Odinga, waligusia zera muhimu ni ya Majimbo, na mheshimiwa Wiliam Ruto Pia aliongelea hapo awali kinaganaga kwenya radio kuhusu sera ya majimbo. Wananchi wanataka mfumo mpya wa utawala. ODM waliongelea masuala matatu, kwanza, uongozi mpya kwa maana ya wananchi kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa maana wameshiriki ufisadi wa nyuma, hivyo hawawezi kufanya mabadiliko yoyote ya maana. Pili; kusafisha mfumo wa utawala kwa maana ya kupambana na rushwa na ufisadi, na tatu, kutengeneza muundo mpya wa utawala ikiwamo kuanzisha muundo wa majimbo. Lakini kwa kuwa suala la majimbo lilipata ladha zaidi na mashambulizi mengi yanatoka kwa wapinzani wetu, wakenya wengechagua chama cha ODM ili sera hii ya majimbo lipewewe jaribio katika taifa letu pia, Suala la sera ya majimbo ni suala la kikatiba. Chama chochote cha siasa kinauza kwa wananchi matakwa yake kama kikipewa ridhaa na wananchi. Matakwa hayo yanaweza kutokana na misingi ya chama husika ama matakwa ya wananchi ama matakwa ya viongozi wa chama husika. suala la kuundwa kwa majimbo ni suala la mabadiliko ya katiba hivyo kwa vyovyote vile ODM itabadilisha katiba kwa haraka sana wakati watakapochukua utawal mwacka ujao. Suala la sera ya majimbo si geni duniani. Nchi kadhaa za Afrika zinafuata mfumo huu, mathalani Afrika kusini, Nigeria, Ethiopia na nyinginezo. Ulaya nchi nyingi zinafuata mfumo huu. Marekani ya Kaskazini, Australia. Kwa kweli dunia kwa ujumla wake inatambua umuhimu wa majimbo. Wengine wamekuwa na majimbo kutokana na tofauti za kimbari/kinasaba (ethnic federalism), wengine ni sababu tu za kurahisisha utendaji (functional federalism) na wengine ni umbali tu wa jiografia (geographical federalism). Kwa hiyo, wote wanaochambua majimbo ni vyema wakachambua pia ufiderali unafanyaje kazi katika nchi hizi, faida na hasara zake. Ukiangalia hata majirani wetu muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni aina ya ufiderali, ingawa ni ufiderali tenge! Nina imani na viongozi wetu na pengine tayari wajadili misingi ya Sera ya majimbo ya ODM na kuangalia vipi ni sehemu ya falsafa ya nguvu ya umma na kwa vipi inaendana na misingi ya ODM, kwa vipi inaweza kusaidia utekelezaji wa sera za ODM na kwa ujumla ni namna gani ni silaha ya nyongeza katika kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi na hatimaye kuleta maisha bora kwa kila MKenya. Kwa mtazamo wangu, hii ni misingi ya “Sera ya majimbo”. Msingi wa kwanza ni kujenga uwezo wa kisiasa, uongozi na uwajibikaji. Sera ya majimbo inaelekeza taifa kuwa na viongozi wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika ngazi mbalimbali. Jinsi Raila alivyo tuelezea katika Uhuru park kwamba hata chiefs watachaguliwa na rahia Uzoefu unaonyesha kwamba kwa kuwa mikono ya mhimili wa serikali ngazi ya chini viongozi hawa wamekuwa sababu ya serikali kuu kuingilia serikali zingine na kimaamuzi na kimwelekeo. Matokeo yake ni kuwa nchi nzima inaendeshwa na Ikulu Nairobi hata katika mambo ya kawaida kabisa. Urasimu huu umekuwa kikwazo cha maendeleo. Nguvu ambayo viongozi hawa wamepewa toka wakati wa muundo wa kikoloni wa kutawala kwa kutumia mawakala umewafanya wawe miungu watu na wanyanyasaji. Kwa kifupi ni watu wasiohitajika. Kwa upande mwingine, sera ya majimbo inataka mameya wachaguliwe na wananchi moja kwa moja badala ya mabaraza ya madiwani ili kuongeza uwajibikaji. Kwa kifupi, msingi huu wa sera unachochea hamasa ya uongozi na kuweka viongozi wenye kuwajibika kwa watu. Hii ndiyo falsafa ya nguvu ya umma katika vitendo. Msingi wa pili ni kushusha na kugawanya madaraka (Devolving and separation of powers). Kwamba uzoefu unaonyesha kuwa majimbo yanapopewa madaraka nayo yanatoa madaraka kwa ngazi ya chini yake na kuendelea mpaka chini kabisa. Serikali kuu inapohodhi mamlaka kadhalika ngazi za chini zinahodhi mamlaka ya ngazi za chini. Hoja inatolewa kwamba je, kwa nini njia isingekuwa serikali huru za mitaa? Hiyo ni njia moja lakini mamlaka (mandate) ya serikali ya mtaa huwa katika maeneo machache, tena ya utekelezaji zaidi tofauti na mfumo wa majimbo. Mfumo wa majimbo unahusisha masuala gani ambayo majimbo yanaweza kuyashughulikia moja kwa moja kama ambavyo masuala yanavyogawanywa kwa misingi ya muungano na yasiyo ya muungano. Lengo ni kuifanya serikali ya fideresheni ishughulike na mambo machache na kila eneo lisimamie mambo yake kwa mujibu wa mazingira ya maeneo husika. Hii ndiyo nguvu ya umma! Msingi wa tatu ni kupanua umoja na mshikamano miongoni mwa WaKenya na kuvunja dhana ya ukabila. Mfumo wa sasa wa kugawa wilaya pamoja na sababu zingine zinazotolewa na serikali umekuwa ukilalamikiwa kuwa umejikuta katika kugawa wilaya kwa mujibu wa makabila-mfano rais Kibaki ameshtuka juzi kuanza kugawa wilaya kule mkoa magaribi na pwani akitafuta nzano kura za wakaaji wa huko mifano ni mingi kweli kweli. Sera ya majimbo imelenga kuvunja mshikamano wa kiwilaya na badala yake kutengeneza fungamano la kimajimbo- mathalani jimbo la Bonde la ufa Riftvaleey linajumuisha makabila yote yanaoyopatikana katika jimbo hilo. Jimbo la Nyanza pegine litaunganishwa na mkoa wa magaribi, na kuwaunganisha watu wote wao kaa magari mwa kenya Lengo ni kutengeneza kizio (unit) kipya cha utambulisho chini ya taifa (Kenya), yaani wakazi wa jimbo fulani na kufanya watu wajinasabishe kabisa na majimbo yao. Hii ni kwa sababu majimbo yanakuwa na upekee wake ambao mtu anapenda ‘kujinasabisha’ nao. Mathalani jimbo moja linaweza kuwa na sheria za ajira zenye kuvutia zaidi, n.k. Hii ndiyo nguvu ya umma! Msingi wa nne ni kuweka utamaduni wa ushindani na upekee ndani ya nchi. Kama ambavyo nchi zinavyoshindana ndivyo ambavyo majimbo yenye taratibu tofauti za kibiashara, ajira, uwekezaji, makazi na kadhalika yatakavyoshindana. Serikali ya majimbo inatoa mwanya wa majimbo kujiamulia mwelekeo wake katika masuala fulani fulani. Mathalani jimbo moja linaweza kupiga marufuku uvutaji sigara; majimbo mengine yanaweza kuiga ama yanaweza kutofuata. Hata katika michezo na kadhalika, ushindani utaongezeka maradufu. Kila jimbo litataka kujifananisha na mafanikio fulani Fulani kwa mfano mkoa wa Nyanza na western yalikuwa yakifuma sana katika kandanda na serikali ilioko sana hivi aijali michezo. Dhana ya ushindani na upekee imeshindikana katika mazingira ya sasa ambapo kila halmashauri inaongozwa na maelekezo ya Nairobi na inajivunia mafanikio ya nchi kwa ujumla wake. Hata binadamu, ukipewa uhuru wa kujiamulia una uwezo wa kufanya vitu vya pekee zaidi kuliko ukiwa sehemu ya mfumo mpana. Hii ni saikolojia ya maendeleo. Hii ndiyo falsafa ya nguvu ya umma! Msingi wa sita ni kupanua vyanzo vya mapato. Pia majimbo yanapopaswa kujitegemea kwa aina Fulani, moja kwa moja yanapaswa kuanza kutafuta njia za kujitegemea. Hii itasaidia vyanzo vya mapato kupatikana. Hii ni kutokana na kanuni ya mwitu (The law of the jungle). Sasa hivi kila mahali wanaitazama Nairobi ikusanye pesa nchi nzima na kutoka kwa wahisani na kila eneo lina achama mdomo kwa ajili ya kupokea! Wapinzani wa sera hii wanatoa hoja kwamba lipo jimbo ambalo halina rasilimali na wanatolea mfano wa jimbo la Kaskazini mashariki (North Eastern). Hawa ni watu ambao pengine hawajui kwamba Kenya ina rasilimali kila mahali. Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa mikoa ya North Eastern haina maendeleo. Ukweli ni kwamba tafiti zinaonyesha mikoa ya kusini ina rasilimali na mali asili nyingi sana, tatizo kubwa ni miundo mbinu. Hata kijana mbunge Khalif alitoka North eastern alionge kwenye mkutano wa Uhuru park akisema kwamba wana mali kama ngombe, mbuzi, ngamia, madini na mengineo Jimbo la pwani (Coast) kwa mfano Jimbo hili lina rasilimali kama madini, bandari, uvuvi, nishati ya gesi, kilimo cha korosho, mikoko pamoja na utalii. ODM likiungana na chama shirikisho ina kila sababu ya kuwaeleza wananchi umuhimu wa majimbo kwani kila jimbo lina rasilimali za kutosha, ila kwa kuwa serikali ya sasa ya rais Kibaki imekuwa ikiwahadaa wananchi na kuwafanya wabweteke kisaikolojia ili wasijiletee maendeleo, imekuwa ikipinga vikali serikali ya majimbo. Hata kama kungekuwa hakuna maliasili: ukweli unabaki kwamba zipo nchi duniani ambazo hazina maliasili lakini zimeneemeka kutokana na kutoa huduma tu! Lakini kwa upande mwingine kama sehemu ya sera ya majimbo, lipo pato ambalo litakusanywa serikali kuu na kusaidia katika maeneo ambayo yana upungufu. Msingi wa saba ni wananchi kunufaika kutokana na matunda ya rasilimali za eneo lao. Mfumo wa sasa ambapo rasilimali zote zinamilikiwa na “Nairobi” kwa maana ya serikali kuu, unafanya wananchi wasinufaike na rasilimali za maeneo yao kikamilifu. Mathalani kodi za madini, mbuga za wanyama nk, sehemu kubwa inakuja serikali kuu na ama kugawanywa katika mfumo ambao haunufaishi maeneo husika ama kutumika katika matumizi ya anasa ya serikali kuu. Mathalani, pamoja na kuvua samaki yanayo safrishwa ng’ambo, Wilaya Homa Bay ni moja ya wilaya maskini kabisa. Wanaofaidi na uvuvi wa samaki yanayo vuliwa ziwa Victoria kupitia wilya Homa Bay wako mji wa Thika ambako viwanda vya samaki yanapatikana. Serikali ya majimbo itakuwa na sehemu ya mamlaka ya ugawanyaji wa mapato yanayotoka katika eneo husika. Pamoja na kukusanya mapato ya pamoja ya serikali kuu. Hii ndiyo nguvu ya umma. Msingi wa nane ni kupunguza ukubwa na gharama za uendeshaji wa serikali. Serikali ya majimbo haiongezi ngazi yoyote ya utendaji kwa kuwa inavunja ngazi ya mkoa (ambayo ni mikoa nane tulizo nazo hapa kenya) na kutengeneza ngazi ya jimbo (majimbo ni machache sina uhakika kwamba ODM itatenga majimbo ngapi, kutegemea na makubaliano ya kikatiba). Wizara nyingine zote zinakuwa katika ngazi ya majimbo husika kwa mujibu wa utaratibu wa majimbo husika. Kutokana na ukaribu wa utoaji huduma na utendaji, mwishowe gharama za utendaji zitakuwa ndogo kuliko Nairobi inavyoendesha nchi mzima katika kila jambo. Mathalani utoaji wa pasi za kusafiria (passport), vibali vya elimu na mambo mengine mengi. Serikali ya majimbo itahakikisha mfumo wa utendaji unakuwa mdogo kwa kujenga mifumo iliyokaribu zaidi. Hii ndiyo nguvu ya umma! Msingi wa tisa ni muundo mpya unaosaidia utekelezaji wa majukumu. Hapa ni mjadala wa kipi kinaanza- muundo ama majukumu (stucture or function). Sera ya majimbo inachukua mtazamo wa kwamba yote yanakwenda pamoja. Wachambuzi wengi wamekuwa wakitoa hoja kwamba matatizo ya msingi ya mwananchi ni hali mbaya ya maisha, kipato duni, uchumi mbovu, elimu duni nk. Na wanachotaka wananchi ni suluhisho la haya matatizo ya msingi si ‘porojo’ za sera ya majimbo. Lakini ukweli ni kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kimatokeo baina ya masuala haya (direct and causality relationship). Mimi ni mwanachama cha ODM katibu mkuu tawi la Kajiado North Daniel Ochieng’ Obunga – 0725-408720 danobunga at yahoo dot com Joluo.com Akelo nyar Kager, jaluo@jaluo.com |
IDWARO TICH? INJILI GOSPEL ABILA
|
Copyright © 1999-2007, Jaluo dot com
All Rights Reserved